Monday, December 31, 2018
TOP 10: Mastaa waliowahi kukiri kuwa Messi ni bora kuliko Ronaldo
Kumekuwa kuna ubishani wa muda mrefu katika dunia ya soka kwa kizazi hiki cha leo kuwa kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi nani ni bora kuliko mwenzake, hii ni mada ambayo imekuwa ngumu kuipatia majibu lakini hii ndio TOP 10 ya mastaa wanaoamini Messi ni bora kuliko Ronaldo.
1- “Kama nitalazimika kuchagua mchezaji mmoja nani bora zaidi ya mwenzake, nitamchagua Messi sababu yupo vizuri katika kutengeneza assist na pasi za mwisho lakini nitakuwa nimempa asilimia 51 kwa 49”>>>Steven Gerrard
Steven Gerrard
2- “Cristiano Ronaldo amekuwa bora na kufanya vizuri duniani lakini Messi yupo juu yake”>>> Ronaldinho
Ronaldinho
3 “Kwangu mimi mchezaji bora duniani ni Lionel Messi”>>> Rafinha
Rafinha
4- “Ningeweza kutaja majina ya wachezaji wengi lakini katika miaka 10 au 15 sasa, nafikiri Messi amekuwa mchezaji bora katika kipindi chote hicho hakuna mashaka Cristiano Ronaldo ni kama Ronaldo wa Brazil anafunga sana lakini kwangu Messi ni bora”>>> Pele
Pele
5- “Nimefanikiwa kukutana na Messi, Ronaldo na Griezmann na nawaheshimu wote ni kweli hawa wote ni bora duniani na tunaweza kutaja wengine pia lakini Messi anacheza kitimu zaidi ya Ronaldo hiyo ndio sababu ya mimi kumuweka juu”>>> Adil Rami
Adil Rami
6- “Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wote ni wachezaji bora duniani lakini Ronaldo hajafikia kiwango cha Lionel Messi”>>> David Beckham
David Beckham
7- “Messi ni bora anajua namna ya kucheza, kufunga na anaweza kuwafanya wachezaji wengine wakacheza vizuri naheshima kwa wachezaji wote lakini naamini Messi yupo level nyingine”>>> Pep Guardiola
Pep Guardiola
8- “Napenda Messi namna anavyocheza kama napewa nafasi ya kuchagua mchezaji mmoja bora basi ni wazi nitamchagua yeye, napenda Messi sababu ni bora lakini hakuna mashaka Ronaldo pia ni mchezaji mzuri”>>> Javier Saviola
Javier Saviola
9- “Kwa mimi ukiniambia nitaje TOP 3 ya wachezaji bora wa muda wote duniani nitasema Messi, Pele na Maradona”>>>
Jose Mourinho
10- “Kuchagu mmoja ni ngumu lakini mimi nitamchagua Messi ni mtu kutoka sayari nyingine na hata Ronaldo pia lakini nafikiri Messi amekamilika zaidi”>>> Ronaldo de Lima
Ronaldo de Lima
Ronaldo vs Messi kwenye El Clasico - Nani mwenye takwimu boraa, rekodi ya magoli na ushindi?
El Clasico, klabu nguli za Hispania Real Madrid na Barcelona zitakapokwaana, ni miongoni mwa mechi kubwa zinazosubiriwa kwa hamu sana kwenye ulimwengu wa soka.
Kule Hispania ni zaidi ya mechi ya soka; ni mtanange wa kiutamaduni, uliogubikwa na itikadi, kadhalika kuonyeshana umwamba baina ya wachezaji wawili bora duniani.
Cristiano Ronaldo dhidi ya Lionel Messi ndilo tukio kuu dunia itakapogeuzia macho pambano hilo, kuamua kwa mara ya tisa, nani mbabe katika mechi hiyo ya miungu wa soka.
Mahasimu hao wanapojiandaa kwa mechi hiyo kubwa, Goal inakuangazia takwimu kuona nani yupo juu ya mwenzake kwenye Clasico.
NANI AMESHINDA MECHI NYINGI ZA CLASICO?
Messi ameshinda mechi ngapi za Clasico?
Mechi | Ameshinda | Sare | Amepoteza |
---|---|---|---|
36 | 16 | 8 | 12 |
Inapokuja kwenye mafanikio ya Clasico, Messi amekuwa upande unaoshinda mara nyingi zaidi ya Ronaldo, akishinda mechi 16 dhidi ya Real Madrid kwenye michuano yote.
Mwargentina huyo amecheza dhidi ya mahasimu wakubwa wa Barca mara 36 kipindi chake cha soka katika michuano tofauti tofauti. Katika mechi hizo 36, Messi ameonja vipigo 12 na kutoa sare nane.
La Liga ndio uwanja wa raha kwenye mafanikio ya Clasico, ushindi 12 kati ya 16 ukipatikana kwenye michuano hiyo.
Kwenye Ligi ya Mabingwa, Messi hajawahi kupoteza mechi kwa Real Madrid, wakiwa wamepata sare na ushindi katika mechi mbili alizoshiriki.
Cristiano Ronaldo ameshinda Clasico ngapi?
Mechi | Ameshinda | Sare | Amepoteza |
---|---|---|---|
28 | 8 | 6 | 13 |
Mafanikio ya Ronaldo kwenye mechi za Clasico yapo chini ukilinganisha na yale ya Messi, lakini ni lazima ifahamike kuwa Mreno huyo amecheza mechi chache, baada ya kujiunga na Real mwaka 2009 - misimu kadhaa baada ya Messi kuanza kuichezea Barca.
Ronaldo amekuwa upande wa ushindi katika mechi nane tu kati ya Clasico 28, akipoteza 13 na kupata sare sita.
NANI AMEFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE CLASICO?
Messi amefunga magoli mangapi Clasico?
Mechi | Magoli | Mashuti | Mashuti yaliyokuwa goli |
---|---|---|---|
36 | 24 | 125 | 19.72% |
Kwa mara nyingine, Messi amekuwa juu kwa mabao aliyofunga kwenye Clasico, akitikisa nyavu mara 24 kwenye mechi 36 baina ya timu hizo.
Magoli mengi yamepatikana La Liga, akiweka kimiani mara 16 katika mechi 22, sita yakipatikana kwenye mechi sita za Supercopa na mawili kwenye Ligi ya Mabingwa.
Michuano pekee ambayo Messi hajafunga dhidi ya Real Madrid ni Copa del Rey baada ya kunyamazishwa kwenye mechi sita.
Magoli mangapi ya Clasico amefunga Ronaldo?
Mechi | Magoli | Mashuti | Mashuti yaliyokuwa goli |
---|---|---|---|
28 | 17 | 117 | 22.5% |
Ronaldo yupo nyuma ya Messi kwa magoli saba kwenye mechi za Clasico akiwa na mabao 17, lakini tofauti hiyo haina maana sana kwani mshindi huyo wa Ballon d'Or amecheza mechi nane pungufu ya hasimu wake.
Uwiano wa Messi wa magoli na mechi ni bora kidogo kuliko wa Ronaldo (0.66 hadi 0.6), ingawa mpinzani wake wa Kireno amejaribu kupiga mashuti mengi zaidi kwa mchezo.
NANI MWENYE PASI NYINGI ZA GOLI?
Messi ametoa pasi ngapi za goli?
Mechi | Pasi za goli | Nafasi alizotengeneza |
---|---|---|
36 | 13 | 65 |
Ronaldo ametoa pasi ngapi za goli kwenye Clasico?
Mechi | Pasi za goli | Nafasi alizotengeneza |
---|---|---|
28 | 1 | 14 |
RONALDO VS MESSI: CLASICO KWA UJUMLA
Mchezaji | Clasico walizoshinda | Magoli | Pasi za goli |
---|---|---|---|
Lionel Messi | 16 | 24 | 13 |
Cristiano Ronaldo | 8 | 17 | 1 |
Amekuwa wa pili nyuma ya Ronaldo kwa mataji na tuzo binafsi mwaka jana, lakini Messi bado ni mfalme wa Clasico.
Mwargentina huyo amefunga magoli mengi zaidi, na kutoa pasi nyingi zaidi za goli na amekuwa upande unaoshinda zaidi Barca inapoikabili Real.
Messi ana uwiano mzuri wa magoli kwa mechi na takwimu zinaonyesha wazi kwamba mchango wake ni mkubwa kwa timu yake Barca kuliko anavyofanya Ronaldo kwa Madrid.
Mshahara wa Mbwana Samatta nchini Ubelgiji huu hapa…
Kufanya kazi Ulaya ni raha sana kwa maana ya kupiga hatua, lakini nako kuna ugumu wake kimaslahi kama utalifikiria suala la kodi. Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza soka mtanzania Mbwana Samatta nchini humo,
Kwa mujibu wa mtandao wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Mshambuliaji mpya wa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa akilipwa mshahara wa euro 35,600 (zaidi ya Sh milioni 85) kwa mwezi.
Lakini makato ya kodi, kupitia kwa Mamlaka ya Kodi ya Ubelgiji, yanamfanya Samatta kuondoka na kiasi kidogo tu cha kodi.
Taarifa za uhakika kutoka Ubelgiji zinasema, Samatta atakuwa akikatwa asilimia 48 kama utajumlisha ‘TRA ya huko’ na makato ya mshahara ya serikali ya mshahara wake. makato ambayo wanakumbana nayo wageni wengi wanaofanya kazi nchini humo.
Pamoja na kulipwa zaidi ya Sh milioni 85, maana yake Samatta atakuwa akipokea euri 18,200 (zaidi ya Sh 38,584).
kabla ya kutua KRC Genk, alikuwa akipokea kitita cha dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 32) kutoka kwa TP Mazembe ambayo aliitumia vizuri kujitangaza.
Maana yake kwa mshahara atakaokuwa akichukua Samatta inaonekana hakuna tofauti kubwa sana na ule aliokuwa akichukua TP Mazembe.
Lakini inawezekana alichoangalia zaidi ni suala la hatua kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi hapo baadaye kimshahara pia kiuchezaji kwa ajili ya kutimiza ndoto zake.
Kwa mwezi huwa inatajwa kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania. Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa hadi euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.
KWa sasa, Samatta ni mwanamichezo anayeshika nafasi ya pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya Hasheem Thabeet ambaye alikuwa akichukua mshahara hadi dola 200,000 kwa mwezi wakati akikipiga ndani ya NBA na sasa hata kama amepunguziwa kwa kuwa yuko ligi ya chini, haiwezi kuwa chini ya dola 100,000 kwa mwezi.
Subscribe to:
Posts (Atom)