Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Burna Boy ameamua kuwatolea uvivu waandaaji wa Tamasha maarufu duniani la Coachella akidai kuwa hawajamtendea haki namna walivyoandikwa jina lake.
Burna Boy kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa yeye ni msanii mkubwa hapa Afrika lakini anashangazwa jina lake kuandika na maandishi madogo na kuchanganywa na wasanii wengine wadogo.
“Nakubali sana kazi zenu Coachella, lakini sikubaliani na namna mlivyoliandika jina langu kwenye tangazo lenu mmeweka maandishi madogo sana. Mimi ni msanii mkubwa barani na siwezi kupunguzwa kwa namna yoyote ile. Nawaomba mbadilishe mapema muwezavyo,“ameandika Burna Boy.
Jana Coachella walitangaza majina ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la hilo na Afrika wametajwa wasanii wawili, Burna Boy na Mr Eazi.
Tangu zamani, Coachella wamekuwa na tabia ya kuandika font size kubwa kwa wasanii wakubwa na size ndogo kwa wasanii wa kawaida.
No comments:
Post a Comment