Wednesday, January 2, 2019

MENEJA WA HARMONIZE (MR PUAZ) ASEPA WCB



MENEJA wa mkali wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize, Mr Puaz ameacha rasmi kazi ya umeneja kwa msanii huyo; kisa ni kutokuwa na maelewano naye.

Baada ya kusikika kwa tetesi hizo Risasi Mchanganyiko lilimtafuta ‘mzee baba’ huyo ili aweze kuzungumzia kusepa kwake na mwelekeo wake mpya wa kikazi.

“Ni kweli kwa sasa mimi na Harmonize hatufanyi kazi pamoja kwa sababu ya kupishana kauli; lakini haimaanishi mimi na WCB hatufanyi kazi au hatutafanya kazi.

“WCB ni familia yangu ambayo ukaribu wangu na wao ulitokana na urafiki wangu na Diamond hivyo siwezi kuiacha, panapo kuwa na nafasi ya mimi kuhitajika kutoa mchango wangu nitaendelea kutoa kama mwanafamilia,” alisema meneja huyo ambapo Harmonize alipotafutwa jitihada ziligonga mwamba kwa sababu simu yake iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment