BAADA ya kila msanii kuoneakana kufanya kazi kivyake, staa wa Bongo Fleva, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ amesema Kundi la TMK Wanaume litarudi na kuanza kazi ya muziki kama lilivyokuwa zamani.
Kuthibitisha hilo, Temba alisema anatarajia kuandaa kolabo moja matata mwaka huu wa 2019 ili kurudisha rasmi kundi hilo.
“Nitawalea wimbo ambao utakuwa na vichwa vyote vya TMK Wanaume niliousimamia mimi, nataka kukata kiu ya mashabiki waliokuwa wanatamani kutuona pamoja,” alisema Temba.
Alisema wanatarajia ujio wao huo kuwa wa tofauti kwa kubadilisha mfumo wa utendaji wa kazi kutoka wimbo kuwa na dakika tano na kuwa dakika tatu.
Kundi la TMK Wanaume lilikuwa likiundwa na mastaa kibao wakiwemo Temba, Juma Nature, Y Dash, Chegge, Inspector Haroun, Dolo, Rich One na KR.
Kundi hilo lilianza kugawanyika kwa baadhi ya mastaa wakiongozwa na Nature, Dolo, Rich One na KR kujitoa kundini na kuanzisha kundi lao la Wanaume Halisi.
No comments:
Post a Comment