Wednesday, January 2, 2019

Dirisha la uhamisho la Januari: Ni nani anayehamia klabu nyengine?

Isco, Paul Pogba, Adrien Rabiot
Ni kelele gani unazoweza kusikia?
Huku tikiingia katika mwaka mpya, mashine ya uvumi wa uhamisho imerudi.
Iwapo unafukuzia kushinda ligi, unataka kupanda daraja, ama kujaribu kuzuia kushushwa daraja, wakufunzi wote watawategemea wenyekiti wa vilabu vyao kuwapatia fedha kuwasajili wachezaji wapya watakaoleta tofauti muhimu katika timu zao.
Paul Pogba , Isco, Adrien Rabiot ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa na uhamisho.
BBC Sport inawaangazia baadhi ya wachezaji ambao huenda wakahama mwezi Januari.

Ligi kuu ya Uingereza

PAUL POGBA (25, kiungo wa kati, Manchester United)
Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe ni maombi ya kutaka kuhamia klabu nyegine?
Anahusishwa na uhamisho wa: Juventus, Barcelona, Paris St-Germain.
Jina kubwa katika orodha yetu.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa mchezaji ghali zaidi wakati alipokuwa akijiunga na Manchester United kutoka Juventus kwa dau la $89m mwaka 2016 amezongwa na ripoti kwamba huenda muda wake katika klabu ya Old Trafford unaisha kwa mara ya pili mwezi huu wa Januari.
Baada ya kuwachwa nje katika kikosi cha kwanza cha United mwezi Disemba , ikiwemo dhidi ya Liverpool , bingwa huyo wa kombe la dunia amevutia klabu kama vile Juventus kukiwa na ripoti za ombi la dau la £125m huku klabu za Barcelona pamoja na PSG zikidaiwa kummezea mate.
Lakini kuondoka kwa mkufunzi Jose Mourinho , ambaye alikuwa na uhusiano mbaya naye, umeinua matokeo ya klabu hiyo ya Old Trafford na inasubiriwa kuona iwapo mchezo wake utazidi kuimarika ama la.
DANNY DRINKWATER (28, kiungo wa kati, Chelsea)
Anahusishwa na uhamisho wa West Ham, Fulham.
Mshindi wa ligi ya Premier , Uhamisho wa Drinkwater hadi Chelsea haikufanyika kwa mpango mzuri- hakuorodheshwa katika kikosi cha mechi za ligi ya Ulaya.
Aliwahi kushirikishwa katika kombe la Community Shiled ambapo Chelsea ilipoteza kwa manchester City na ameambiwa na mkufunzi maurizio Sarri kwamba anweza kuondoka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chelsea anaweza kuongeza nguvu katika safu ya kati na uwezekano wa yeye kujiunga tena na mkufunzi wake wa zamani Claudio ranieri katika klabu ya Fulham upo juu.
GARY CAHILL (33, beki, Chelsea)
Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, AC Milan, Aston Villa, Fulham.
Cahil ni mchezaji mwengine wa Chelsea ambaye ameshindwa kunazishwa katika kikosi cha kwanza chini wa ukufunzi wa mkufunzi Maurizio Sarri, Cahill hachezeshwi na ameambiwa yuko huru kuondoka.
Akiwa na kiwango cha juu cha uzoefu katika klabu na kimataifa pamoja na kuishindia Chelsea makombe mengi, Cahil hawezi kukosa maombi kutoka vilabu vikubwa ndani ya ligi ya Uingereza, vilabu bingwa na hata pengine klabu za ligi ya Serie A nchini Itali.
Kwengineko bayern Munich wameripotiwa kuwasilisha ombi la $21m kumsajili kinda wa Chelsea Calklum Hudson-Odoi, huku wachezaji w enza kama vile CEsc Fabregas, Victor Moses na Andreas Christensen pia wakitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo.
BRAHIM DIAZ (19, kiungo wa kati, Manchester City)
Brahim Diaz
Diaz atakamilisha kandarasi yake msimu huu na anakasirishwa na kukosa kuchezeshwa.
Mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja wa wachezaji wachanga wa taifa hilo wenye mafanikio makubwa siku za usoni na huenda akafuata Jadon Sancho kwa kujaribu bahati yake nje ya lkigi ya Premia.
Ripoti kutoka uhispania zinasema kiuwa mabingwa wa ligi hiyo Real Madrid wamekubaliana na mchezaji huyo kwa uhamisho wa dau la £13.6m huku mchezaji huyo akitarajiwa kupokea mishara wa £60,000 kwa wiki.
JERMAIN DEFOE (36, mshambuliaji, Bournemouth)
Anahushishwa na uhamisho : Crystal Palace, Nottingham Forest, Sheffield United, Wigan.
Mchezaji wa Uingereza wa zamani Defoe amekuwa hachezeshwi msimu huu akishiriki dakika 30 pekee katika ligi ya Uingereza.
Akiwa amefunga magoli 162, Defoe ni mfungaji mzuri na anaweza kucheza kwa muda mfupi kwa ytimu inayohitaji mshambuliaji licha ya umri wake.
DOMINIC SOLANKE (21, mshambuliaji, Liverpool)
Anahusishwa na uhamisho wa : Crystal Palace, Huddersfield, Brighton.
Solanke, ambaye ameichezea Uingereza mara moja, hajapokea nafasi ya kuiwakilisha Liverpool , baada ya kushindwa kuonyesha mchezo mzuri.
Pia tunaangalia iwapo kipa Simon Mignolet atasalia Anfiled , huku mchezaji huyo wa Ubelgiji akiwa wa pili nyuma ya Alisson.
ADRIEN SILVA (29, kiungo wa kati, Leicester)
Anahusishwa na uhamisho wa: Sporting Lisbon.
Oumar NiasseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWill Niasse sign for Cardiff or Huddersfield?
Anahusishwa na uhamisho wa : Cardiff, Huddersfield, Crystal Palace.
Niasse alifunga magoli manane akiichezea Everton msimu uliopita lakini sasa amekuwa akicheza kama mchezaji wa ziada na amecheza mechi nne pekee katika ligi na sasa ameorodjheshwa miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuondoka katika klabu hiyo.
Huku Niasse akiwa amesajiliwa kwa dau la £13m mwaka 2016 , mkufunzi Marco Silva atalazimika kukubali dau la chini ili kuweza kumuuza mshambuliaji huyo wa Senegal , ambaye anaweza kunoa makali ya safu za ushambuliaji za Cardiff na Huddersfiled.
Mchezaji mwenza James McCarthy amerudi katika hali yake baada ya kuvunjika mkuu mara mbili na pia huenda akaruhusiwa kuondoka kwa mkopo.
Max AaronsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Anahusishwa na uhamisho wa : Tottenham, RB Leipzig.
Licha ya kuanza kucheza mwezi Agosti, kinda wa Norwich Aaron amedaiwa kuwa beki bora chipukizi katika ligi ya manbingwa nchini Uingereza. mchezo mzuu wa timu yake umevutia klabu za ligi kuu ya uingereza Tottenham ambao wanaweza kuwasilisha ombi la £15m pamoja na klabu ya Ujerumani RB Leipzig.
NEAL MAUPAY (22, mshambuliaji, Brentford)
Anahusishwa na uhamisho wa: Huddersfield.
Brentford huenda inang'ang'ania kusalia katika ligi hiyo ya mabingwa , lakini mchezaji wa Ufaransa Maupay amekuwa aking'ara baada ya kufunga magoli 14 na kutoa usaidizi wa magoli mengine sita msimu huu.
Huku Huddersfield ikiwa ndio timu yenye magoli machache katika ligi ya Uingereza , Maupay anaweza kutoa usaidizi mkubwa wa magoli kwa dau la a £10m move.
JARROD BOWEN (22, winger, Hull)
Anahusishwa na uhamisho wa : Cardiff, Fulham, Leeds.
Mchezaji mwengine anayeonyesha mchezo mzuri katika timu isiojiweza kimchezo.
Bowen alikuwa mchezaji wa Hull na mchezaji anayeoungwa mkono na mashabiki wa klabu hiyo na amefunga magoli manane katika kampeni hiyo.
Je winga huyo atafurahia kutondoka katika klabu ya Hull na kujiunga na klabu kama vile Cardiff ama Fulham ambao wanapata shida katika ligi kuu ya Uingereza?
LLOYD KELLY (20, defender, Bristol City)
Anahusishwa na uhamisho : Liverpool, Manchester United.
Mchezaji wa timu ya vijana ya Uingereza Kelly amekuwa mchezaji bora katika ligi hiyo ya ligi ya mabingwa.
Akielezewa na meneja Lee Johsnon akama mchezaji hatari, kelly mwenye kasi kubwa huenda akajiunga na klabu moja katika ligi kuu iwapo ataendelea na mchezo huo mzuri.
Wachezaji walio huru
Image captionWachezaji walio huru


Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp, na zinazokaribia kufungiwa

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp, simu nyingi za smartphone zilikuwa za Blackberry na Nokia
Wamiliki wa simu zinazotumia programu endeshi ya simu aina ya Series 40 wamekuwa hawawezi tena kutumia mtandao wa WhatsApp kwenye simu zao.
Hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp wa kuacha kutengeneza app yake kwa njia ambayo inaweza kutumiwa katika simu hizo.
Wengi zaidi wataathirika katika kipindi cha mwaka ujao, 1 Februari, 2020 ambapo simu nyingi zikiwemo baadhi ya iPhone zitapoteza uwezo wa kutumia WhatsApp.
Hata kabla ya wakati huo kufika, Facebook wameonya kwamba "kwa sababu hatutakuwa tukitengeneza na kuboresha app yetu tukizizingatia, huenda baadhi ya uwezo wake ukaathirika wakati wowote."
Zitakazoathirika mwaka ujao ni za Android zinazotumia Android 2.3.7 na miundo ya awali, pamoja na iPhone zinazotumia iPhone iOS 7 kwenda nyuma. Kwa sasa, mfumo wa Android umefikia 9.0. [Unaweza kuangalia mfumo unaotumiwa na simu yako kwenye 'Settings', kisha sehemu ya 'Software/Software Info]
Wanaotumia Android 2.3.7 kwenda nyuma hawawezi kufungua akaunti mpya za WhatsApp.
Ndipo uweze kutumia mtandao huo kwa sasa unahitajika kuwa unatumia Android 2.3.3 kwenda juu na Windows Phone 8.1 kwenda juu.
Kwa sasa, walioathirika zaidi ni wanaotumia baadhi ya simu za Nokia zinazotumia mfumo endeshi wa Series 40 ambao wakati mwingine huitwa S40 OS. Miongoni mwa simu maarufu zilizoathirika ni Nokia 6300.
Nokia 6300Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSimu aina ya Nokia 6300
Simu ya mwisho kutegenezwa ambayo ilikuwa inatumia S40 ilikuwa Nokia 515 ambayo ilizinduliwa mwaka 2013.
Ingawa baadhi ya simu hizi ni za bei nafuu na hutumiwa na watu wa kipato cha wastani au cha chini, kuna wanaotumia simu aina ya pia simu za Vertu Signature S ambazo zilikuwa ghali sana na ambazo hutumia programu hiyo endeshi pia.
Wakati wa kuanza kuuzwa kwa simu hizo zilikuwa zinauzwa takriban £8000 (Tshs23m; Kshs1m), ingawa hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita na huenda wengi wao wamenunua simu nyingine au wana uwezo wa kununua simu nyingine kwa urahisi.

Simu zilizoathirika kwa sasa

  • Nokia 206 Single SIM na dual SIM
  • Nokia 208
  • Nokia 301 Single SIM na dual SIM Chat Edition
  • Nokia 515 zinazouzwa zikiwa na WhatsApp
  • Nokia Asha 201
  • Nokia Asha 205 Chat Edition
  • Nokia Asha 210
  • Nokia Asha 230 Single SIM na dual SIM
  • Nokia Asha 300, 302, 303, 305, 306, 308, 309, 310, 311
  • Nokia Asha 500, 501, 502, 503
  • Nokia C3-00
  • Nokia C3-01
  • Nokia X2-00
  • Nokia X2-01
  • Nokia X3-02
  • Nokia X3-02.5
Simu ambazo haziwezi kutumia WhatsApp na tarehe ya kuacha kutumia
  • Nokia Symbian S60 baada ya Juni 30, 2017
  • BlackBerry OS na BlackBerry 10 baada ya Desemba 31, 2017
  • Windows Phone 8.0 na miundo ya awali Desemba 31, 2017
  • Nokia S40 baada ya Desemba 31, 2018
  • Android 2.3.7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
  • iPhone iOS 7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020

Simu nyingine zisizotumia WhatsApp

Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."
Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.
Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.
Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.
WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja dunianiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawawezi kutumia WhatsApp:
  • Android 2.1 na Android 2.2
  • Windows Phone 7
  • iPhone 3GS/iOS 6
  • BlackBerry OS and BlackBerry 10
  • Nokia S40
  • Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.
Simu ya BlackberryHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSimu ya Blackberry
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Forbes: Floyd Mayweather ndio mwanamichezo tajiri zaidi duniani


Floyd Mayweather v Conor McGregorHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMayweather (kushoto) na McGregor walizipiga katika pigano lao la raudni 10 mwezi Agosti 2017

Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.
Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ua masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.
Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.
La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.
Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema
Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.
Mayweatjher ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m
"Mechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400m'' , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.
"Lakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn
Aliongezea: "Orodha ya Forbes' ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.

  1. Floyd Mayweather - Ndondi ($285m)
  2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
  3. Cristiano Ronaldo -kandanda($108m)
  4. Conor McGregor - Karate, judo na Ndondi ($99m)
  5. Neymar - kandanda ($90m)
  6. LeBron James - Vikapu ($85,5m)
  7. Roger Federer - tenisi ($77.2m)
  8. Stephen Curry - Vikapu ($76.9m)
  9. Matt Ryan - Soka ya Marekani ($67.3m)
  10. Matthew Stafford - Soka ya Marekani ($59.5m)